Sunday, July 25, 2010

WANAJESHI WALIOPIGANA VITA KUU WAILALAMIKIA SERIKALI

WAZEE WALIOPIGANA VITA YA PILI WALALAMIKA KUTORIDHIKA NA WALIVYOTENDEWA NA SERIKALI



Richard Mwangulube,Arusha

Wananchi wa Mkoa wa Arusha leo wameadhimisha siku ya mashujaa kwa kupambwa na gwaride la gadi moja ya jeshi la mgambo wakiongozwa na bendi ya Chuo cha jeshi nchini[TMA] kilichopo Monduli.


Maadhimisho hayo yamefanyika mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenye mnara wa kumbukumbu ya askari wa waliopigana katika vita vya Kagera.


Wakati wa maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa huo Jowika Kasunga (Monduli) , Raymond Mushi( Arusha)Mercy Silla( Arumeru) Elias Wawalali ( Ngorongoro) na James Ole Millya wa Longido pamoja na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na jiji la Arusha .


Sherehe hizo pia zimehudhuriwa na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama mkoani hapa pamoja na Kamati za ulinzi na usalama, watendaji wakuu wa idara ya Serikali na taasisi za Umma.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isidore Shirima aliweka ngao na mkuki, mshauri wa mgambo S.S. Mkumbo aliweka upinde, wakati askari wa mstaafu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ),Kanali Mstaafu Gunzu aliweka shoka.


Askari aliyepigana vita kuu ya pili mwenye namba T 946 mzee Eliam Mrabundi aliweka sime katika mnara huo wakati Mkurugenzi wa Jiji Raphael Mbunda yeye aliweka Maua.


Hata hivyo akizungumz amara baada ya kuhitimishwa kwa shughuli hizo, mzee Eliam Mrabundi ambaye alipigana vita kuu ya pili ameelezea maskitiko yake na kudai kuwa pamoja na mchango wao huo lakini hadi leo hii hawajalipwa fedha zao tangu aliporejea Nchini kutoka Misri mara baada ya kumalizika kwa hiyo.


Aidha Mzee huyo ameelezea masikitiko yake hayo na kwamba hata baada ya uhuru Serikali imeshindwa kuthamini mchango wa wazee hao waliotetea nchi na baadhi yao kupoteza maisha yao

Nao askari wastaafu wa JWTZ wamesema pamoja na kushiriki katika harakati za kulinda nchi na kujitolea kwanda Msumbiji na kupigana katika vita vya Kagera lakini wengi wao hawajalipwa fedha zao hadi sasa.

1 comment:

  1. ni muhimu nao wakatendewa haki kama ilivyo kwa wastaafu wa taasisi nyingine za umma kwani wengi wamechoka

    ReplyDelete