Richard Mwangulube Arusha
Wagombea Udiwani wa UWT kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arumeru wamepiga matokeo yaliyotangzwa jana wakati wa Uchaguzi wa Jumuiya hiyo ya Chama kwa madai kuwa Uchaguzi huo ulitawaliwa na mizengwe pamoja na ubabe.
Wagombea hao pamoja na baadhi ya Wanachama wa Jumuiya hiyo ya wapatao 23 tayari wamewasilisha rufaa yao kwa katibu wa CCM wa mkoa wa Arusha na nakala kupelekwa kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Taifa, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Arusha pamoja na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU) .
Katika kupinga matokeo hayo wamesema uchaguzi huo uliendeshwa bila kuzingatia kanuni , taratibu na sheria zinazoongoza shughuli za uchaguzi ndani ya jumuiya hiyo ama Chama cha Mapinduzi.
Aidha Walalamikaji hao wamesisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi huo ulikuwa na mwelekeo mzima wa kuwepo na upangaji wa matokeo kutokana na kuendeshwa kwa ubabe.
Wamesema wakati wa kuhesabu kura wagombea walikataliwa kutuma wawakilishi wao kwa ajili ya kushuhudia kura zao pia baadhi ya watendaji wa UWT wilaya akiwemo katibu wa UWT Wilaya waliendelea kusimamia shughuli za uchaguzi licha ya watendaji hao kuwa wagombea.
Msimamizi wa uchaguzi alitoa matokeo tofauti na yalivyokuwa na kusababisha mshangao katika ukumbi huo kutokana na kubabaika na hivyo wametaka uchaguzi huo kurudiwa tena ama kura kuhesabiwa upya.
Katibu wa UWT Wilaya Frida Kaaya alipotafutwa kwa njia ya simu hakuweza kupatikana kabisa wakati Katibu wa UWT Mkoa wa Arusha Elly Minja alipohojiwa kwa njia ya simu alisema hilo ni jukumu la Wilaya na sio la Mkoa.
mwisho
No comments:
Post a Comment